Maswali 160 na Majibu kwaajili ya Maandalizi ya Mtihani
wa Konstebo wa Idara ya Uhamiaji.
YALIYOMO.
Nyaraka hii ina jumla ya maswali 160
pamoja na majibu yake, yaliyotayarishwa mahsusi kwa ajili ya maandalizi ya
mtihani wa maandishi wa nafasi ya Konstebo wa Idara ya Uhamiaji. Maswali yameandaliwa
kwa kuzingatia majukumu halisi ya kazi ya uhamiaji, mazingira ya vituo vya
mipakani, viwanja vya ndege, bandari, na ofisi za uhamiaji.
Maudhui yake yanajumuisha mada mbalimbali
zikiwemo uraia na uhamiaji, mipaka ya Tanzania, historia ya taifa, maadili na
nidhamu ya utumishi wa umma, usalama wa mipaka, nyaraka za kusafiria, taratibu
za uingiaji na utokaji, pamoja na hali za dharura kama vita, majanga na
wakimbizi. Aidha, maswali mengi ni ya kiuchambuzi na hali halisi ili kumsaidia
msomaji kuelewa namna ya kufanya maamuzi sahihi kazini, si kukariri majibu
pekee.
Nyaraka hii imelenga kuwasaidia waombaji
kutoka taaluma na sifa tofauti kujijenga kitaaluma, kuongeza uelewa wa kazi ya
uhamiaji, na kuongeza nafasi ya kufaulu katika mtihani wa maandishi kwa
kujiandaa kwa kina na kwa uelewa mpana wa majukumu ya Konstebo wa Uhamiaji.
Imeandaliwa na
Johnson Yesaya – Mwanasheria..
0628729934.
02/02/2026.
Ndugu Waombaji Kazi,
Mkusanyiko huu wa maswali na majibu
umeandaliwa kwa umakini ili kuwasaidia kuelewa maeneo muhimu yanayopimwa katika
mtihani wa maandishi wa nafasi ya Konstebo wa Idara ya Uhamiaji. Maudhui yake
yamelenga kutoa mwongozo wa vitendo na unaoendana na majukumu halisi ya kazi ya
uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi sahihi katika mazingira ya kazi.
Lengo kuu ni kuwawezesha kujiandaa kwa
kujiamini, kukuza uelewa wa kitaaluma, na kushiriki katika mchakato wa usaili
kwa ufanisi. Nakutakieni maandalizi mema.
Disclaimer - Maswali haya ni ya maandalizi
tu, hayajatolewa wala kuidhinishwa na Jeshi la Uhamiaji Tanzania.
1. Tanzania inapakana na nchi ngapi kwa upande wa nchi kavu?
A. Nchi 6 B. Nchi 7 C. Nchi 8 D. Nchi 9
Jibu sahihi: C
Maelezo:
Tanzania inapakana na
nchi 8 kwa nchi kavu: Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbiji.
2. Mipaka ya Tanzania kwa upande wa
bahari ipo katika bahari ipi?
A. Bahari ya Hindi B. Bahari ya Atlantiki C. Bahari ya Mediterania D. Bahari
Nyekundu
Jibu sahihi: A
Maelezo: Tanzania ina mpaka wa bahari katika
Bahari ya Hindi upande wa Mashariki.
3. Tanzania Bara ina mikoa mingapi kwa
sasa?
A. Mikoa 25 B. Mikoa 28 C. Mikoa 27 D. Mikoa 26
Jibu sahihi: D
Maelezo: Tanzania Bara ina mikoa 26, baada ya
kuanzishwa mikoa mipya kama Geita, Katavi, Songwe na Simiyu.
4.
Zanzibar ina mikoa mingapi?
A. 3 B. 4 C. 5 D. 6
Jibu
sahihi: C
Maelezo:
Zanzibar ina mikoa 5: Kaskazini Unguja,
Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba.
5. Uraia wa Tanzania hupatikana kwa
misingi ipi mikuu?
A. Kuzaliwa, kuolewa, kuajiriwa B. Kuzaliwa, kurithi, kuhamia C. Kuhamia,
kuandikishwa, uraia wa hiari D. Kuzaliwa, kurithi, na tajinisi
Jibu sahihi: D
Maelezo: Uraia wa Tanzania hupatikana kwa misingi
mikuu mitatu: uraia wa kuzaliwa, ambapo mtu huzaliwa na wazazi raia wa
Tanzania; uraia wa kurithi, ambapo mtoto hupata uraia kupitia mzazi wake
raia; na uraia wa tajinisi, ambapo raia wa kigeni hupewa uraia baada ya
kuishi Tanzania kwa muda unaotakiwa kisheria na kutimiza masharti
yaliyoainishwa. Misingi hii ndiyo inayotambuliwa rasmi kisheria na hutumika
katika masuala ya uhamiaji na uraia.
6. Nani alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
A. Rashidi Kawawa B. Edward Sokoine C. Julius Nyerere D. Cleopa Msuya
Jibu sahihi: A
Maelezo: Baada ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar mwaka 1964, Rashidi Kawawa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa
kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7. Edward Moringe Sokoine alikuwa
anashikilia wadhifa upi wakati wa kifo chake?
A. Rais B. Makamu wa Rais C. Waziri Mkuu D. Spika wa Bunge
Jibu sahihi: C
Maelezo: Edward Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa
Tanzania alipofariki mwaka 1984.
8. Msafiri hana tiketi ya kurudi wala
uthibitisho wa safari ya kuendelea. Hii inaashiria nini?
A. Ni jambo la kawaida kwa wasafiri wote
B. Inaweza kuashiria hatari ya kukaa kinyume cha masharti
C. Ni kosa la jinai moja kwa moja
D. Haihusiani na uamuzi wa uhamiaji
Jibu sahihi: B
Maelezo: Kukosa mpango wa kuondoka ni kiashiria
cha hatari kinachohitaji uchunguzi wa ziada.
9. Nchi ipi kati ya hizi HAIPAKANI na
Tanzania?
A. Zambia B. Ethiopia C. Rwanda D. Malawi
Jibu sahihi: B
Maelezo: Ethiopia haipakani na Tanzania; nchi
jirani za Tanzania ni 8 kwa nchi kavu.
10. Wizara inayosimamia masuala ya
Uhamiaji ni ipi?
A. Wizara ya Ulinzi B. Wizara ya Mambo ya Nje C. Wizara ya Katiba na Sheria D. Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Jibu sahihi: D
Maelezo: Idara ya Uhamiaji iko chini ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
11. Konstebo wa Uhamiaji anapofanya kazi
kituo cha mpakani, jukumu lake la msingi ni lipi?
A. Kudhibiti uhalali wa kuingia na kutoka nchini B. Kukusanya ushuru wa forodha C.
Kusajili mali za wasafiri D. Kutoa vibali vya kazi kwa wageni
Jibu sahihi: A
Maelezo: Kazi ya msingi ya Konstebo ni
kuhakikisha wanaoingia au kutoka nchini wanatimiza masharti ya uhamiaji. Hii
inahusisha kukagua nyaraka na kufuata taratibu za uingiaji/utokaji, si
kukusanya ushuru, kusajili mali, au kutoa vibali maalum.
12. Raia wa kigeni anawasili akiwa na
pasipoti halali lakini anakosa visa inayohitajika. Hatua sahihi ni ipi?
A. Kumruhusu aingie kwa masharti maalum B. Kuzuia kuingia na kumuelekeza afuate
taratibu C. Kumshtaki papo hapo kwa kosa la jinai D. Kumruhusu akaombe visa
ndani ya nchi
Jibu sahihi: B
Maelezo: Bila visa sahihi, uingiaji nchini haukidhi masharti. Hatua
stahiki ni kuzuia kuingia na kumwelekeza afuate taratibu husika, si kumruhusu
kwa masharti yasiyo halali wala kumshtaki papo hapo bila msingi.
13. Nyaraka zipi husaidia zaidi
kuthibitisha uraia wa Tanzania kwa mhusika?
A. Leseni ya udereva pekee B. Kadi ya bima ya afya C. Cheti cha kuzaliwa pamoja
na kitambulisho cha taifa D. Barua ya serikali ya mtaa peke yake
Jibu sahihi: C
Maelezo: Uraia unathibitishwa vyema kwa
mchanganyiko wa nyaraka rasmi zinazoaminika. Cheti cha kuzaliwa na kitambulisho
cha taifa hutoa uthibitisho thabiti kuliko nyaraka za ziada zisizo za uraia.
14. Konstebo akigundua jaribio la rushwa
wakati wa ukaguzi, hatua ipi inaendana na maadili ya utumishi wa umma?
A. Kukataa kimya kimya na kumruhusu aende B. Kukubali na kuharakisha taratibu C.
Kumzuia bila kurekodi tukio D. Kukataa, kurekodi tukio, na kutoa taarifa kwa
mamlaka
Jibu sahihi: D
Maelezo: Maadili yanataka kukataa rushwa,
kurekodi tukio, na kutoa taarifa. Hii inalinda uadilifu wa idara na huzuia
mianya ya ukiukwaji.
15. Lengo kuu la udhibiti wa mipaka ni
lipi?
A. Kulinda usalama na maslahi ya taifa B. Kuongeza idadi ya wageni C.
Kurahisisha biashara ya ndani D. Kupunguza kazi za idara nyingine
Jibu sahihi: A
Maelezo: Udhibiti wa mipaka unalenga usalama wa
taifa na maslahi ya umma. Faida nyingine zinaweza kuwepo, lakini si lengo kuu.
16. Mgeni aliyeruhusiwa kukaa kwa muda
maalum akikaa zaidi bila ruhusa, hali hiyo inaeleweka vipi?
A. Ni kosa dogo lisilohitaji hatua B. Ni ukiukwaji wa masharti ya kukaa nchini C.
Ni ruhusa ya kuomba uraia D. Ni haki ya msingi ya mgeni
Jibu sahihi: B
Maelezo: Kukaa zaidi ya muda ulioruhusiwa ni ukiukwaji wa masharti ya
uhamiaji na huchukuliwa hatua kulingana na taratibu.
17. Msafiri anadai amepoteza pasipoti
lakini hana uthibitisho wowote. Hatua ipi ni sahihi?
A. Kumruhusu aingie kwa maelezo ya mdomo
B. Kumzuia bila uchunguzi
C. Kuomba uthibitisho wa ziada kwa taratibu
D. Kumruhusu aende bila kumbukumbu
Jibu sahihi: C
Maelezo: Taarifa za kupotea lazima zithibitishwe
kabla ya uamuzi.
18. Konstebo anapokabidhiwa hati za
kusafiria, hatua ya kwanza sahihi ni ipi?
A. Kuuliza maswali ya safari bila kukagua B. Kuangalia umri wa msafiri pekee C.
Kuweka muhuri mara moja D. Kukagua uhalali na uhalisia wa hati
Jibu sahihi: D
Maelezo: Ukaguzi wa uhalali na uhalisia wa hati
ni hatua ya kwanza kabla ya hatua nyingine zozote za kiutawala.
19. Ni hali ipi inaweza kuashiria hatari
ya usalama wa mpaka?
A. Mgeni mwenye maelezo yanayokinzana kuhusu safari B. Msafiri mwenye tiketi ya
kurudi C. Msafiri aliye na mizigo midogo D. Raia mwenye nyaraka kamili
Jibu sahihi: A
Maelezo: Maelezo yanayokinzana yanaweza kuashiria
hatari au jaribio la kuficha taarifa muhimu, hivyo huhitaji umakini zaidi.
20. Ushirikiano kati ya Uhamiaji na
vyombo vingine vya ulinzi ni muhimu kwa sababu gani?
A. Kupunguza majukumu ya Konstebo B. Kuimarisha usalama na ufanisi wa
utekelezaji C. Kuongeza taratibu zisizo za lazima D. Kubadilishana majukumu
kikamilifu
Jibu sahihi: B
Maelezo: Ushirikiano huongeza ufanisi na usalama
kwa kubadilishana taarifa na kuratibu hatua, bila kuvuruga majukumu ya msingi.
21. PCCB ni kifupi cha taasisi ipi?
A. Ofisi ya Kuzuia Rushwa B. Bodi ya Udhibiti wa Rushwa ya Umma C. taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa D. Ofisi ya Udhibiti na Uzingatiaji wa Umma
Jibu sahihi: C
Maelezo: PCCB ni kifupi cha taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Taasisi hii ina jukumu la kuzuia, kuchunguza
na kupambana na vitendo vya rushwa katika sekta ya umma na binafsi, na ni nguzo
muhimu katika kuimarisha maadili, uwajibikaji na uadilifu katika utumishi wa
umma.
22. Konstebo anapokutana na msafiri wa
mpito (transit traveler), anapaswa kuzingatia nini zaidi?
A. Uraia wa msafiri B. Muda na masharti
ya mpito C. Idadi ya mizigo D. Sababu ya kusafiri awali
Jibu sahihi: B
Maelezo: Wasafiri wa mpito wanazingatiwa kwa
masharti maalum ya muda na njia.
23. Tanzania ina mpaka wa ziwa na nchi
zipi kati ya hizi?
A. Kenya na Uganda B. Uganda na Rwanda C. Malawi na Msumbiji D. Burundi na
Zambia
Jibu sahihi: A
Maelezo: Tanzania inapakana kwa njia ya Ziwa
Victoria na Kenya na Uganda.
24. Ni ipi tofauti kati ya “visa” na
“kibali cha ukaazi”?
A. Visa ni ruhusa ya kudumu, kibali ni cha muda mfupi B. Visa ni ruhusa ya kuingia/kuwasili, kibali cha ukaazi ni ruhusa ya kukaa kwa
muda maalum C. Visa hutolewa ndani ya nchi tu, kibali hutolewa mpakani tu D. Visa ni kwa raia pekee, kibali ni kwa wageni pekee
Jibu sahihi: B
Maelezo: Visa mara nyingi huonyesha ruhusa ya
kuingia/kuwasili kwa lengo maalum, wakati kibali cha ukaazi kinahusu ruhusa ya
kukaa nchini kwa muda na masharti yaliyowekwa.
25. Uraia wa nchi nyingine kwa raia wa
Tanzania unaruhusiwa kwa masharti gani?
A. Bila masharti B. Kwa ruhusa ya serikali C. Tanzania hairuhusu uraia pacha
kwa ujumla D. Kwa kuolewa pekee
Jibu sahihi: C
Maelezo: Kwa ujumla, Tanzania haitambui uraia
pacha isipokuwa kwa mazingira maalum yanayotambuliwa kisheria.
26. Msafiri anasema anakuja “kutembea”
kwa siku 7, lakini ana nyaraka zinazoashiria anatafuta kazi. Konstebo afanye
nini?
A. Kumruhusu aingie kwa kuwa muda ni mfupi B. Kumkatalia kwa sababu tu
“anatafuta kazi” C. Kuuliza maswali ya uthibitisho na kuchunguza ulinganifu wa
nyaraka na maelezo D. Kumruhusu aingie na kumwambia asitafute kazi
Jibu sahihi: C
Maelezo: Tofauti kati ya maelezo na nyaraka ni
kiashiria cha hatari/ukiukwaji wa masharti; maswali ya uthibitisho na
ulinganisho wa nyaraka huwezesha uamuzi wa haki na taratibu.
27. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) inasimamia mambo yapi zaidi?
A. Mambo yote ya Muungano B. Uhamiaji wa Bara C. Ulinzi wa taifa lote D. Mambo
yasiyo ya Muungano Zanzibar
Jibu sahihi: D
Maelezo: SMZ inasimamia mambo yasiyo ya Muungano
upande wa Zanzibar.
28. Wizara ya Ulinzi inasimamia taasisi
ipi?
A. Jeshi la Polisi B. Jeshi la Uhamiaji C. JWTZ D. PCCB
Jibu sahihi: C
Maelezo: JWTZ iko chini ya Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa.
29. Uhamiaji haramu unaathiri taifa kwa
njia ipi?
A. Huongeza idadi ya watu tu B. Huathiri usalama, ajira na huduma za jamii C.
Huongeza mapato ya serikali D. Huimarisha diplomasia
Jibu sahihi: B
Maelezo: Uhamiaji haramu una athari pana
kiusalama, kiuchumi na kijamii.
30. Mkoa upi una mpaka wa bahari kati ya
hii?
A. Morogoro B. Kigoma C. Pwani D. Mbeya
Jibu sahihi: C
Maelezo: Mkoa wa Pwani una mpaka wa Bahari ya Hindi.
📘 Pata PDF Kamili ya Maswali ya Mtihani wa Uhamiaji Kupitia Gmail Yako (Swali 1–160)
Umesoma maswali 30 ya mwanzo. Seti kamili ya maswali 160 ya kujiandaa na mtihani wa uhamiaji yanapatikana kwa malipo ya Tsh 10,000. Fanya malipo na upate PDF kamili mara moja kwenye Gmail yako.
Fanya Malipo ya Tsh 10,000 kwa namba zaifuatazo:
Baada ya malipo, tume message ya muamala kutufahamisha kwamba umefanya malipo kwaajili ya maswali ya kujiandaa na mtihani wa uhamiaji.
⚠️ TAARIFA MUHIMU
PDF utakayopokea itawekwa jina lako na namba ya siri, na imelindwa kwa matumizi binafsi pekee.
Hairuhusiwi kabisa:
kusambaza kwa mtu mwingine
kupiga screenshot
kunakili maudhui yoyote
Ukisambaza kinyume cha sheria, jina lako na namba yako vitaonekana wazi na ni rahisi kufuatilia chanzo cha uvujaji wa nyaraka.
Hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya nakala hii.
.png)
0 Comments
PLACE YOUR COMMENT HERE
WARNING: DO NOT USE ABUSIVE LANGUAGE BECAUSE IT IS AGAINST THE LAW.
THE COMMENTS OF OUR READERS IS NOT OUR RESPONSIBILITY.